REA yaja na mpango wa kuvifikia vijiji vyote

0
132

Wakala wa nishati vijijini (REA) imesema wamesema ina mpango wa kuhakikisha wanafikisha umeme kwenye vitongoji ili kuwezesha watanzania hususani wanaoishi vijijini kutumia fursa ya umeme katika uzalishaji mali.

Akizungumza katika maonesho ya 46 ya kimataifa ya Dar es salaam,Mkurugenzi wa huduma za ufundi kutoka REA, Mhandis Jonsu Olotu amesema REA inalenga kuwatengenezea fursa za ufanyaji biashara wananchi kupitia nishati ya umeme ili waweze kuongeza thamani ya mazao ambayo yatawawezesha kushiriki kikamilifu kwenye eneo huru la Biashara barani Afrika.

Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya REA Mhandisi Francis Hongera amesema REA inampango wa kusambaza zaidi umeme vijijini kutoka asilimia 62 ya sasa.