RC Mtaka atangaza neema kwa walimu

0
329

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ametoa ofa kwa walimu wa shule za msingi na sekondari watakaobuni teknolojia ya njia ya mtandao kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi ambao wako majumbani kwa sasa.

Mtaka ameyasema hayo wakati akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju katika kuhitimisha mafunzo ya msaada wa kisheria kwa wanawake viongozi na wasio viongozi mkoani simiyu.

Amesema atakuwa tayari kuwasaidia walimu watakaobuni teknolojia ili watumie fursa hiyo kufikisha masomo kwa wanafunzi wa madarasa ya mitihani ambao wako majumbani kwa sasa.