Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza kuwa kuanzia Jumatatu, Aprili 20, 2020 kila anayekwenda sehemu ya manunuzi, lazima avae barakoa na kuwataka wafanyabiashara kufanya biashara zote kwa njia ya ‘take away’ ili kuepusha watu kukaa kwa mkusanyiko katika maeneo hayo.
Makonda ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akieleza mikakati ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona ambapo hadi sasa visa 147 vimethibitishwa nchini.
“Anayekwenda eneo la manunuzi yotote lazima awe amevaa barakoa (mask), ununue, ukate leso, ukate kanga utaamua wewe, lakini lazima uwe umevaa.
“Pia kuanzia Jumatatu biashara zote zifanyike katika mfumo wa ‘take away’ ukienda sehemu nunua ondoka, lazima pia kuwe na hatua mita mbili katika msongamano wa watu,” amesema Makonda
Aidha, amewataka wenye masoko kutumia njia mbadala wa kufanya kazi kwenye masoko yao ili kujikinga na corona