RC MAKALLA AUTAKA USHIRIKA WENYE TIJA KWA TAIFA

Vyama vya Ushirika

0
187

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha wanaanza kuwawezesha Maafisa ugani na Ushirika wa Mkoa huo ili waweze kutimiza majukumu yao kitaifa na kutembelea miradi ya Ushirika na sio kusota maofisini.

Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la nne la Ushirika jijini Dar es salaam

Pamoja na hayo RC Makalla amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa nia yao ya dhati ya kuboresha na kuimarisha Ushirika nchini.