RC Kunenge: Watendaji wa mitaa shughulikieni kero za wananchi

0
266

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amewataka Viongozi ngazi Mitaa kuhakikisha wanashughulikia ipasavyo kero na changamoto mbalimbali kwenye mitaa yao

Kunenge ameyasema hayo wakati wa kikao chake na Watendaji na Wenyeviti wa mitaa Jijini dar es salaam ambapo amesema ni Jambo la fedheha kuona kiongozi wa ngazi ya juu anashughulikia kero ya mtaa wakati wahusika wa ngazi ya mtaa wapo.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewaelekeza Watendaji wa Mkoa huo kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ukusanyaji wa Mapato ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya vya Mapato, kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ambapo ametaka ukusanyaji wa Mapato usiwe wa kero Wala wa kuua Biashara za watu.

Hata hivyo amewataka Viongozi wa Mitaa kusimamia ipasavyo suala la usafi wa mazingira kwenye mitaa yao ili kuwakinga wananchi na magonjwa ya Mlipuko.

Pamoja na hayo Kunenge amewasisitiza pia Viongozi hao kutoa taarifa pindi wanapobaini uwepo wa watu wanaohatarisha usalama ikiwemo kufichua nyumba zinazogeuzwa Madanguro