RC Kigoma awajulia hali Zitto Kabwe na wenzake

0
480

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amefika katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Kigoma kuwajulia hali majeruhi waliopata ajali ya gari katika msafara wa wagombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini na Kigoma Kusini kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe na Said Bakema, mtawalia.

Rais Magufuli amjulia hali Zitto Kabwe baada ya ajali

Ajali hiyo ilitokea baada ya gari ya ACT-Wazalendo kuigonga gari nyingine na kupinduka, magari hayo yalikuwa kwenye msafara wa kampeni ndani ya jimbo la Kigoma kusini, wilaya ya Uvinza katika eneo la Kijiji cha Lufubu, kata ya Kaly.

Katika ajali hiyo watu 11 wamejeruhiwa na kupatiwa matibabu katika Kituo cha afya Kalya ambapo sita wameruhusiwa huku watano wakipewa rufaa kwenda kwenye hospitali hiyo.

Zitto Kabwe apata ajali mkoani Kigoma

Taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Simon Chacha, inasema watu watano wamepokelewa katika hospitali ya rufaa ambapo wagonjwa wote wanaendelea vizuri ila Zitto Kabwe ameomba rufaa ya kwenda Muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi kutokana kujihisi maumivu katika bega lake la kushoto.