RC Gaguti : Marufuku kuwatoza fedha wakulima

0
149

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti amepiga marufuku wakulima wa korosho mkoani humo kutozwa fedha ili wagawiwe pembejeo za bure zilizotolewa na serikali.

Brigedia Jenerali Gaguti ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Libobe, alipokuwa akikagua zoezi la upuliziaji wa pembejeo zilizotolewa bure na serikali ambako kumeibuka changamoto hiyo ya wakulima kutozwa fedha pindi wanapohitqji kupatiwa pembejeo.

Amesema serikali imetoa vitabu maalum kwa ajili kuandikisha taarifa za mkulima, hivyo mkulima hapaswi kutoa kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya zoezi la ugawaji wa pembejeo hizo.

Kwa mujibu wa RC Gaguti, kumtoza fedha mkulima katika zoezi hilo ni kwenda kinyume na utaratibu mzima wa maelekezo ya serikali na kwamba kuanzia sasa hakuna mkulima yoyote ndani ya mkoa wa Mtwara kutozwa kiasi chochote cha fedha kwa kisingizio cha shajara na mambo mengine.