RC Chalamila : Tuwekeze kwa vijana

0
125

Mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila amewataka vijana kote nchini kuwa na mipango ya kiuchumi, kijamii na kimaendeleo wakati bado wakiwa na nguvu, huku wakizingatia nidhamu na uzalendo kwa Taifa lao.

Chalamila ametoa wito huo wakati wa kongamano la vijana lililofanyika mkoani Kagera.

“Zisake fursa uwezavyo wakati bado ukiwa kijana na wakati sahihi, kwani maisha yako ya mbeleni yanategemea na vile ambavyo umejiandaa tangu ukiwa kijana.” amesema Chalamila

Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Kagera ametoa wito kwa vijana nchini kuendelea kuwa wazalendo na kutimiza majukumu yao mapema kabla muda haujapita, huku akiwataka viongozi kuwekeza kwa vijana

Akizungumzia wiki ya vijana, Chalamila amewataka vijana kuyatumia maonesho yaliyoandaliwa kuzungumza na Vijana wenzao wa Kagera na kuona fursa mbalimbali zilizopo za uwekezaji na ujasiriamali .

Chalamila amewaomba wazazi na viongozi nchini kuendelea kuwapa fursa vijana pamoja na nafasi ya kusikilizwa na kushirikishwa kwenye maamuzi mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa kuwa viongozi bora wa baadaye.