Rais Samia Suluhu Hassan amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella, kukaa meza moja na viongozi wa kimila wa jamii ya kimasai ili kuweka sawa, changamoto zilizopo kwenye hifadhi ya Ngorongoro ambapo ndani yake kuna jamii zina makazi.
“Nataka kuwaahidi malaigwanani namleta mkuu wa mkoa aje kukaa nanyi, yakimshinda nitaingia mwenyewe nitakuja mwenyewe na tuone tunatokaje pale tulipo ni kweli Ngorongoro ni muhimu.”- Rais Samia Suluhu Hassan.
“Tunapozungumza Arusha na Utalii Ngorongoro ni muhimu sana hatuwezi kwenda na matakwa ya watu na tukaua Ngorongoro, Haiwezekani Ngorongoro lazima ibaki na watu waendelee kuishi lakini maisha yamo ndani ya hifadhi peke yake ? hapana hata nje kuna maeneo tunaweza kutoa watu wakakaa, Malaigwanani tutakuja kuwasikiliza mtusaidie ili tuondoshe migogoro,”-Rais Samia Suluhu Hassan.