Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ameiomba wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kuruhusu mwanamume kuingia na mke wake kwenye chumba cha kujifungulia pindi anapomsindikiza kujifungua.
Brigedia Jenerali Mstaafu Maganga ametoa ombi hilo mkoani Kigoma katika hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la mafunzo kwa vitendo katika chuo cha uuguzi wilayani Kibondo na kuongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza umoja na mshikamano kwa wazazi wa mtoto atakayezaliwa.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa wa Kigoma, hatua hiyo pia itapunguza malalamiko ambayo yamekua yakitolewa dhidi ya Watumishi wa sekta ya afya kuwa, baadhi yao wamekua wakitoa lugha isiyofaa kwa akinamama wanaokwenda kujifungua.
