Rapa Pop Smoke auawa kwa risasi

0
148

Rapa kutoka nchini Marekani, Bashar Barakah Jackson maarufu kama Pop Smoke amefariki dunia kwa kupigwa risasi mjini Los Angeles.

Pop Smoke ameuawa akiwa na umri wa miaka 20 kwa kupigwa risasi Jumatano Februari 19 katika mazingira yaliyoonekana kuwa ni uvamizi nyumbani kwake, Hollywood Hills.

Lebo ya muziki inayosimamia kazi za Pop Smoke, Republic Records, imetuma salamu za pole kwa familia, marafiki na mashabiki kwa kuondokewa na rapa huyo chipukizi.