Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Mcha Hassan Mcha kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kabla ya uteuzi huo, Mcha alikuwa Kamishna wa Udhibiti na Utekelezaji (Control and Enforcement), Makao Makuu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Mcha anachukua nafasi ya Msafiri Lameck Mbibo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Madini.
Uteuzi huu umeanza tarehe 5 Desemba, 2021.
Aidha, Rais Samia amemteua Balozi Celestine Joseph Mushy kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria.
Balozi Mushy alikuwa Katibu Tawala Msaidizi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Uteuzi huu umeanza tarehe 14 Januari, 2022.