Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto amewasili nchini akipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax ambapo atafanya ziara ya siku mbili.
Rais Ruto ameambatana na mke wake Rachel Ruto wakati akiwasili nchini.
Rais Ruto anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Oktoba 10, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo kutakuwa na matukio mbalimbali.
Hii ni ziara ya kwanza nchini tangu kuapishwa kuwa Rais wa Kenya Septemba 13 mwaka huu.