Rais ziarani mkoani Morogoro

0
356

Rais Samia Suluhu Hassan kesho anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Morogoro.

Akizungumzia ujio wa ziara hiyo ya kwanza kufanyiwa na Rais, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shigela amesema akiwa mkoani humo Rais atazungumza na wananchi ambapo amewaomba wakazi wote wa mkoa wa Morogoro kujitokeza ili kumpokea kiongozi huyo.

“Ninawaomba wakazi wa mkoa wa Morogoro kujitokeza kwa kuwa ziara hii ya Rais ni ziara ya kwanza tangu kuiangia kwake madarakani,” amesema.

Aidha, Shigela amesema Rais atashiriki mkutano mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania utakaofanyika Julai 8 katika Manispaa ya Morogoro.