Rais Yoweri Museveni awataka watanzania kuthamini maendeleo yakitaifa

0
454

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewataka watanzania kuunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania za kuwekeza kwenye miundombinu itayofaidisha watu wote.

Museveni amemshukuru Rais Magufuli kwa kujenga reli na uwanja wa ndege mkubwa wa Chato utakao rahisisha na kuunganisha shughuli za kibiashara kati ya Tanzania na Uganda.

Katika ziara yake hiyo ya siku moja nchini Tanzania Rais Museveni ameahidi kujenga vyumba vya madarasa saba katika kijiji cha Nyamirezi kilichopo wilaya ya chato jirani na ulipo uwanja wa ndege huo wa Chato.