Rais : Wanawake unganeni kupinga unyanyasaji

0
152

Wanawake nchini wametakiwa kuungana na kushirikiana, ili kuondoa unyanyasaji unaoendelea kwa baadhi ya Wanawake.

Akizungumza na Wanawake wa Tanzania kupitia kwa Wanawake wa mkoa wa
Dodoma, Rais Samia Suluhu Hassan amesema anashangaa kuona sheria na miongozo ipo kuhusu kuzuia unyanyadaji huo lakini bado unaendelea katika baadhi ya maeneo nchini.

Amesema wakati umefika kwa Wanawake nchini kujitathmini ni wapi ambapo mambo hayajakaa vizuri na wapi wamelegalega na kuruhusu kuendelea kwa unyanyasaji dhidi yao.

Rais Samia Suluhu Hassan amewashauri Wanawake nchini kutumia majukwaa ama madawati yaliyoundwa kwa ajili ya kushughulikia masuala yao, ili pamoja na mambo mengine yasaidie kuondoa unyanyasaji dhidi yao.

Kwa mujibu wa Rais Samia Suluhu Hassan, unyanyasaji unaoendelea miongoni mwa Wanawake kwa namna nyingine unaathiri makuzi ya Wasichana ambao watakaokuwa akina mama hapo baadae.