Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi amuapisha Katibu wake

0
571

Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi  amemuapisha Suleiman Ahmeid Saleh kuwa Katibu wa Rais wa Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi amemuapisha Katibu huyo  baada ya  kumteua Novemba 4, mwaka huu kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Viongozi mbalimbali wamehudhuria hafla hiyo iliyofanyika Ikulu, Zanzibar, akiwemo Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi Talib Haji, Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Hassan Khatib, Naibu Kadhi Mkuu, Sheikh Hassan Othman Ngwali, Viongozi wa Vikosi vya SMZ  pamoja na  viongozi mbalimbali kutoka idara na taasisi za Serikali.

Kabla ya uteuzi huo katibu huyo  alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Tume ya Pamoja ya Fedha.