Rais wa Iran awaonya askari wa mataifa ya kigeni

0
335

Rais wa Iran, Hassan Rouhani amewaonya askari wa mataifa ya kigeni hasa kutoka barani Ulaya walioko katika eneo la Mashariki ya Kati na nchi za kiarabu kuwa ni vema wakaondoka katika eneo hilo kwa usalama wao.

Rouhani amesema askari hao wanaweza wakajikuta kwenye shida au wamepata maafa kwa vile nchi hiyo inapambana na adui aliyehatarisha usalama nchini Iran.

Hivi karibuni nchi ya Iran ilishambulia kwa makombora kambi za majeshi ya Marekani zilizopo Iraq hali ambayo imeanza kutishia usalama katika eneo hilo la nchi za kiarabu.

Hata hivyo nchi za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, zimeionya nchi ya Iran kuwa imeanza kukiuka mkataba wa amani wa nyuklia wa nchi hiyo wa mwaka 2015.