Rais Shein ateta na Waziri Zungu

0
185

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amemuhakikishia ushirikiano Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mussa Azzan Zungu katika kutekeleza majukumu yake.


Dkt Shein ameyasema hayo Ikulu Zanzibar alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Zungu na kumhakikishia majukumu yake hasa ya Muungano atampa ushirikiano wa kutosha.


Rais Shein amemueleza kiongozi huyo kuwa, miongoni mwa majukumu yake ni kuhakikisha jitihada za waasisi, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume za kuleta Muungano zinaendelezwa.


Naye Waziri Zungu ameahidi kufanya kazi kwa ufanisi kwa maslahi mapana ya nchi.