Rais Samia: Watu wajiandae kuhesabiwa

0
217

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Watanzania kujiandaa na sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 2022.

Rais Samia ametoa rai hiyo katika uzinduzi wa mkakati wa uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Pia, ametoa wito kwa Mamlaka ya Takwimu kutumia weledi wao na kuhesabu watu waliopo ndani ya mipaka ya nchi.