Rais Samia: Watanzania msiwe na hofu kuhusu chanjo wa Uviko -19

0
151

Rais Samia Suluhu Hassan amesema asingekuwa tayari kuhatarisha maisha yake kwa kuchanjwa chanjo ya covid kama ingekuwa si salama.

Rais Samia ameyasema hayo leo Julai 28, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Chanjo ya Uviko -19 na zoezi la utoaji wa chanjo hiyo, lililofanyika Ikulu Dar es Salaam.

Hatua hiyo inakuja baada ya wiki iliyopita Tanzania kupokea zaidi ya dozi milioni 1.05 za chanjo aina ya Johnson & Johnson zilizotolewa na Marekani kupitia mpango wa upatikanaji wa chanjo Covax.

Rais Samia alisema yeye ni mama wa watoto wanne, ni bibi wa wajukuu kadhaa wanaompenda sana na yeye kuwapenda, ni mke pia lakini mbali ya yote ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi wa nchi hii.

“Nategemewa kama mama, kama bibi, kama Rais, kama Amiri Jeshi Mkuu, nisingejitoa mwenyewe nikajipeleka kwenye kifo, nikajipeleka kwenye hatari nikijua kwamba nina majukumu yote haya yananitegemea .