Rais Samia: Wanawake ni muhimu kwenye maendeleo

0
258

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kundi la wanawake lina nafasi kubwa katika kuchangia maendeleo ya Taifa kupitia shughuli mbalimbali wanazofanya katika jamii.

Rais Samia ameyasema hayo katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa kumpongeza katika utendaji kazi wa miezi sita, uliofanyika katika viwanja vya Maisara visiwani Zanziibar, ambapo amesisitiza kuwa ili Taifa lisonge kimaendeleo, wanawake wanapaswa kujua wajibu wao katika maendeleo.

“Tuliambiwa na wajuzi wa uchumi kuwa uchumi ni mambo matatu, uwe na ardhi, mtaji, lakini pia uwe na wafanyakazi. Kwa upande wetu hatukuwa na mtaji na ardhi lakini nguvu kazi tunayo kama wanawake wanaweza kufanya kazi, kwa hiyo serikali zetu zimetuwezesha sasa kuwa ana ardhi na kuwa na mtaji, kilichobaki sasa ndugu zangu ni kuchapa kazi,”-amesema Rais Samia.

Amesema mambo mengine Serikali inaendelea kuweka mazingira bora ili kuwezesha kufanya kazi ikiwepo kufufuliwa kwa majukwaa ya wanawake.

Ameongeza kuwa sheria zinaendelea kuboreshwa ili kumpa mwanamke haki sawa za kupata huduma zote za kijamii ikiwemo kupata elimu na afya.