Rais Samia: Wanasheria tendeni haki

0
71
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wajumbe wa Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki (East Africa Law Society) kabla ya kufungua Mkutano wa 27 wa Chama hicho uliofanyika Jijini Arusha tarehe 24 Novemba, 2022.

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wanasheria kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa na kutoa haki kwa watu wanaowahudumia.

Rais Samia ameyasema hayo jijini Arusha alipokuwa akifungua mkutano wa 27 wa chama cha Wanasheria wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALS).

Amesema kutotenda haki ni kuwaadhibu watu wasiostahili na kuwafanya waishie kutumikia vifungo wasivyostahili gerezani.

“Kwenye haki peke yake ndio mataifa hustawi.” amesisitiza Rais Samia

Pia amewapongeza wanachama hao wa EALS kwa kufikisha miaka 27 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya yao.

Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza EALS kuweka kipaumbele katika maslahi ya Taifa na kuongeza kuwa yupo tayari kufanya kazi na chama hicho.

Aidha, Rais Samia amesema suala la Tanzania kurudi kuwa mwanachama wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu litachukua muda hadi kufikiwa kwa uamuzi.

“Unaweza ukawa na mwanamke mrembo, tabia zake kwako zikawa sizo, utakaa naye?, utampa nafasi mpaka akajirekebishe. Sisi tunajirekebisha kwetu na wao wajirekebishe kwao kisha tutarudi kwenye ushirikiano.” amesema Rais Samia