Rais Samia : waliosemwa sana kwenye rushwa ni wanasiasa

0
138

Rais Samia Suluhu Hassan amesema amefuatilia maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Afrika na kubaini wanasiasa ndio wametajwa sana kwenye vitendo vya rushwa, wakifuatiwa na wafanyabishara huku vyombo vya Ulinzi na Usalama navyo vikiguswa.

Rais Samia amesema hayo jijini Arusha katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Barani Afrika.

“Nadhani wote walioshiriki hapa tumeona kwa takwimu, na nilikuwa naona pia picha zikioneshwa rushwa zilivyoshamiri katika maeneo hayo. Kwa hiyo wale wote waliohusika kwenye maeneo haya tutafuatilia maazimio ya mkutano huu na twende tukafanye marekebisho”. Amesema Rais Samia

Ameeleza kufurahishwa baada ya kuona kundi kubwa la vijana kuanzisha klabu za kupambana na rushwa mashuleni, vyuoni na hata waliohitimu wameanzisha klabu nje ya taasisi hizo za elimu na wanaendelea na mapambano dhidi vitendo vya rushwa.