Rais Samia: Waliopo kwenye huduma za utalii wachanje

0
152

Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka wadau wote wanaojihusisha na utoaji wa huduma za kitalii wachanje, ili waweze kufanya kazi kwa uhuru bila kuwekewa vikwazo vyovyote.

Rais Samia Suluhu Hassan, amezungumza hayo jijini Arusha akiwa na ziaraya kikazi mkoani humo.

“Tanzania tulikuwa kwenye orodha ya nchi ambazo hazitembeleki wala hatujadiliwi ulimwenguni kwa sabau ya UVIKO -19, lakini juzi mmesikia baada ya jitiada tulizozichukua tumetolewa kwenye orodha ile na Tanzania sasa ipo safi na wameshapeana ruhusa ya kuja kututembelea”- amesema Rais Samia Suluhu Hassan.

“Tunachofanya kingine ni jitihada ya kufanya watu wetu wote ambao wapo kwenye huduma za kitalii na wenyewe wachanje ili kujenga imani kwa wageni wanao kuja kwamba watu wetu wanao wahudumia pia wamechanja,”- ameongeza Rais Samia Suluhu Hassan.