Rais Samia: Uimara wa nchi ni kujitegemea

0
169

Rais Samia Suluhu Hassan, ameeleza kuwa tozo zitaendelea, na umuhimu wa tozo ni maendeleo ya nchi.

Rais Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kilimanjaro katika ziara yake ya kikazi ambayo imeambatana na uzinduzi wa miradi mbalimbali.

“Udume wa mwanaume ni kujitegemea na umahiri wa nchi ni kujitegemea, kama nchi lazima tuwe na chanzo chetu cha kuboresha elimu na sekta ya Afya, na Tozo zimeleta maendeleo,”-Rais Samia Suluhu Hassan.

“Tumeanzisha Tozo hizi za miamala ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu tayari tumekwenda kujenga vituo maeneo mbalimbali na madarasa 500 yanajengwa kwa hiyo tozo zetu tunaendelea nazo,”- ameongeza Rais Samia Suluhu Hassan.