Rais Samia: Tutunze Mlima Kilimanjaro

0
160

Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka wananchi wa Kilimanjaro kutunza mlima Kilimanjaro, na mazingira ili sifa ya mlima huo isipotee kutokana na kuyeyuka kwa barafu ambayo ameshuhudia wakati akirekodi makala ya Royal Tour.

Rais Samia Suluhu Hassan, amezungumza hayo katika mkutano wa hadhara mkoani humo akiwa katika ziara ya kikazi ambayo imeambatana na uzinduzi wa miradi mbalimbali.

Pia Rais Samia Suluhu Hassan amewasisitizia wananchi wa Kilimanjaro kuwa shughuli za binadamu ni muhimu na lazima lakini pia uhifadhi wa mazingira ni lazima.