Rais Samia: Tutaendelea kukopa kwa manufaa ya Taifa

0
119


Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kukopa kwa ajili ya ujenzi wa miradi yenye manufaa na maendeleo kwa taifa.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR Lot 6) kipande cha kutoka Tabora kwenda Kigoma, Dkt. Samia amesema, pamoja na baadhi ya watu kupinga hatua ya serikali kukopa pesa kwenye mashirika ya kimataifa lakini hawataacha kukopa kwa manufaa ya taifa.

“Lazima niseme ukweli mradi huu tunauendesha kwa mikopo na tunakopa kwa ajili ya maendeleo na si vinginevyo,” amesema Dkt. Samia

“Nataka niseme kidogo, hizi trilioni 23.3… za kitanzania zote ni mikopo, kwa hiyo wale wanaosema awamu hii wamekopa sana ndio awamu iliyojenga reli yote,” ameongeza Dkt. Samia

Ameongeza kuwa zaidi ya shilingi bilioni 227.8 zimetumika kama mishahara kwa wafanyakazi 20,000 wanaofanya kazi kwenye mradi huo.