Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wakazi wa Babati mkoani Manyara na Watanzania wote kutilia mkazo sekta ya kilimo, kwani ni moja ya sekta muhimu nchini.
“Tuongeze jitihada kwenye kilimo. Manyara ni mkoa wa kiimo ni mkoa unaolima mazao mengi, niwaombe sana wananchi kuendeleza juhudi za kilimo.” amesema Rais Samia
Akizungumza na wananchi wa mkoa wa Manyara katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kwaraa, Babati, Rais Samia pia amewahimiza kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.