Rais Samia Suluhu Hassan: Nikikuta mabango kiongozi umekwenda

0
318

Rais Samia Suluhu Hassan amewaagiza Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali aliowaapisha hii leo kufanya kazi kwa kutenda haki na sio kuwanyanyasa wanaowaongoza.

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo Ikulu jijini Dar es salaam alipokuwa akiwaapisha viongozi hao na kuongeza kuwa katika uongozi wake hatapenda kuona viongozi anaowateua wanawanyanyasa wanaowaongoza na jambo hilo likitokea ataamua vinginevyo.

Kuhusu kero mbalimbali za Wananchi, Rais Samia Suluhu Hassan ametaka kushughulikiwa kwa kero hizo kwa uharaka na si kusubiri viongozi wakuu akiwemo yeye mwenyewe, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.

Amesema katika ziara zake akiona bango la malalamiko ya Wananchi na utatuzi wa jambo hilo liko ndani ya uwezo wa viongozi wa ngazi ya chini, Mkuu wa wilaya ama Mkurugenzi wa  halmashauri ataondolewa katika wadhifa wake.