Rais Samia Suluhu Hassan kulihutubia Bunge

0
140

Rais Samia Suluhu Hassan atalihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 22 mwezi huu siku ya Alhamisi.

Spika wa Bunge, -Job Ndugai ameliambia Bunge jijini Dodoma kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan atalihutubia Bunge kuanzia saa 10 jioni.

Spika Ndugai amewataka Wabunge wote walioko nje ya jiji la Dodoma kurejea jijini humo kwa ajili ya kusikiliza hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia Suluhu Hassan analihutubia Bunge kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufuatia kifo cha Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano.