Rais Samia Suluhu Hassan atuma salamu za Ramadhani

0
199

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewatakia Waislamu wote mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Rais Samia Suluhu Hassan, amewaomba Waislamu kuiombea nchi amani, upendo, mshikamano na utulivu ili kujenga mazingira bora zaidi kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

Ibada ya funga itaanza kesho Aprili 14, 2021 kwa Waislamu, ikiwa ni moja ya nguzo za Uislamu.