Rais Samia Suluhu Hassan ateta na Spika

0
171

Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Mazungumzo hayo yamefanyika huku Rais Samia Suluhu Hassan
akitarajiwa kulihutubia Bunge Alhamisi wiki hii, majira ya saa 10 jioni.

Hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan itakuwa ni ya kwanza Bungeni tangu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Machi 19 mwaka huu, kufuatia kifo Dkt. John Magufuli.