Rais Samia Suluhu Hassan: Acheni mijadala isiyo na afya

0
367

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujikita katika kazi iliyo mbele yao kwa sasa ya kupitisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 na kuachana na mijadala ambayo haina afya kwa Taifa.

Amesema mijadala inayoendelea hivi sasa katika mitandao mbalimbali ya kijamii na kuhamia Bungeni ya kumlinganisha yeye na Hayati Dkt. John Magufuli kwa sasa si wakati wake.

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dodoma, wakati wa kongamano maalum lililoandaliwa na viongozi wa dini nchini kwa lengo la kumshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya Dkt. Magufuli na kuwaombea Viongozi waliopo.