Rais Samia Suluhu Hassan : Acheni kujiingiza kwenye migogoro

0
218

Rais Samia Suluhu Hassan amewaonya Wakuu wa mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kutojihusisha kwenye migogoro ya ardhi na atakayefanya hivyo atachukuliwa hatua za kinidhamu.

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa onyo hilo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Tawala wa mikoa aliowateua hivi karibuni.

Amesema kuwa kamwe hatavumilia kuona Viongozi anaowateua wanajiingiza kwenye migogoro ya ardhi na kuwa sehemu ya kuwaumiza Wananchi badala ya kuwasaidia kutatua migogoro hiyo.

Rais Samia Suluhu Hassan pia amewataka Viongozi hao kwenda kushughulikia migogoro ya mirathi, na kuongeza kuwa katika eneo hilo kumekuwa na uonevu mkubwa hasa kwa Wanawake na Watoto.

Amewataka kushughulikia migogoro ya aina hiyo, huku wakizingatia sheria na kwa kuzingatia masuala muhimu yanaowahusu wahusika hasa dini.