Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Afrika
Julai 11, 2023 jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Kamishna Salum Hamduni amesema hayo jijini Arusha wakati akitoa taarifa ya ufunguzi wa maadhimisho hayo ya siku tatu yanayoanza leo Julai 09, 2023 hadi Julai 11, 2023 mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla.
