Rais Samia mgeni Rasmi miaka 45 ya CCM

0
156

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi siku nne Mkoani Mara ambapo pamoja na mambo mengine, atashiriki katika Maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama cha mapinduzi (CCM).

Rais atawasili Februari mjini Musoma Februari 4, na Februari 5 ataongoza sherehe za maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kisha kuanza ziara ya kikazi februari 6.

Katika ziara yake, Rais atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya Kimkakati pamoja na kuzungumza na Wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Akizungumzia ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi, amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi katika maeneo yote ambayo Rais anatarajiwa kupita.

Hapi amesema kwa mapenzi ya mama kwa Wananchi wake, anatagemea kuongea nao (kuhutubia) katika maeneo atakayopita.