Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Dodoma tayari kuongoza shughuli ya kitaifa ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma, Rais amepokelewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa na viongozi wengine wa serikali.
Akiwa mkoani Dodoma Rais Samia ataongoza viongozi wa serikali kuupokea mwili wa Dkt. John Magufuli ambapo baada ya kuwasili mwili huo utapelekwa Ikulu ya Chamwino na utalazwa hapo.
Jumatatu Machi 22, 2021 Rais atawaongoza Watanzania na wageni kutoka mataifa mbalimbali katika shughuli ya kitaifa ya kuuga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.