Rais Samia kushuhudia ujazaji maji Bwawa la Nyerere

0
153

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio la kushuhudia ufungaji wa lango la handaki mchepuko (diversion tunnel) ili kuruhusu maji yaanze kujaa katika bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere litakalofanyika Desemba 2022.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati, January Makamba mara baada ya kutembelea mradi huo uliofikia asilimia 78.68 ambapo bwawa hilo lina uwezo wa kuhifadhi lita bilioni 33.2 za maji na kama zikitumika na mitambo yote itaweza kuendesha mitambo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande amesema itachukuwa misimu miwili ya mvua kulijaza bwawa hilo na kuanza kujaribu mitambo ambapo licha ya faida ya kupata umeme lakini mradi huo una faida kwenye kilimo chini ya Mto Rufiji na kuondoa mafuriko.