Rais Samia kushiriki mazishi ya Malikia Elizabeth

0
304

Rais Samia Suluhu Hassan amewasili jijini London nchini Uingereza, kushiriki katika mazishi ya Malkia Elizabeth II wa nchi hiyo yatakayofanyika tarehe 19 mwezi huu.

Katika uwanja wa ndege wa Luton,
Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na mwakilishi wa Mfalme Charles III wa Uingereza,
Cynthia Gresham pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo Dkt. Asha -Rose Migiro .