Rais Samia Suluhu Hassan, leo anaendelea na ziara yake ya kikazi siku nne mkoani Kigoma.
Kwa siku ya leo atasimama katika eneo la Mvungwe akitokea Kibondo kuelekea Kasulu na kusalimia wananchi wa eneo hilo.
Rais Samia pia atafungua chuo cha Ualimu Kabanga na kuzungumza na wananchi.
Kazi nyingine itakayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan akiwa mkoani Kigoma, ni kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Manyovu – Kasulu – Kibondo – Kabingo/Kakonko na kufungua barabara ya Kidahwe – Kasulu.
Atazindua umeme wa Gridi ya Taifa, na kufungua ofisi ya mkuu wa wilaya Buhigwe.
Rais Samia Suluhu Hassan yupo mkoani Kigoma ambapo anatembelea, kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo mkoani humo na kuzungumza na wananchi wa mkoa huo.