Rais Samia kufanya ziara Kigoma

0
226

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Kigoma, kuanzia tarehe 16 hadi 19 mwezi huu.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ziara hiyo, mkuu wa mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amesema kuwa, ziara ya Rais Samia itaanzia wilayani Kakonko.

Amesema akiwa mkoani Kigoma, pamoja na mambo mengine Rais Samia atafungua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo .

Aidha Andengenye amewataka wakazi wa wilaya za mkoa wa Kigoma ambazo Rais atapitia zikiwemo za Kakonko , Kibondo Kasulu, buhigwe na Kigoma kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo.

Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Kigoma ni ya kwanza tangu aingie madarakani mwezi Machi mwaka 2021.