Rais Samia: “January nakuelekeza”

0
247

Rais Samia Suluhu Hassan ameielekeza wizara ya Nishati inayoongozwa na waziri January Makamba kuhakikisha ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mapema mwaka 2023, nishati safi inasambazwa kwenye taasisi kubwa.

“Wakati nikiwa Makamu wa Rais, na nina bahati na January kwenye mambo ya mazingira. Kule nilimuelekeza taasisi zinazohudumia zaidi ya watu 300 lazima watumie nishati safi… akiwa kule hakukaa muda mrefu akatoka hatukulitekeleza. Nakuelekeza tena leo, lilelile kwamba taasisi zile; jela, shule, vikosi vya ulinzi zianze sasa kujielekeza kwenye nishati safi ya kupikia.” ameagiza Rais Samia

“Sasa hivi sihesabu, mwaka mzima wa 2023 nataka mjielekeze kwenye hili la taasisi kubwa kutumia nishati safi.” amesisitiza Rais Samia

Alikuwa akifungua Mjadala wa KItaifa wa Nishati Safi ya Kupikia unaofanyika kwa muda wa siku mbili mkoani Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa nishati.