Rais Samia aweka jiwe la msingi ujenzi wa uwanja wa ndege Iringa

0
181

Rais Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa ndege wa Iringa, ujenzi utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 60 hadi kukamilika kwake.

Akizungumza baada ya kuweka jiwe hilo la msingi Rais Samia amesema kiwanja hicho kitasaidia kusafirisha mazao nje ya nchi, kwani Iringa ni moja ya mikoa inayozalisha mazao ya biashara.

Leo Rais Samia Suluhu Hassan anamaliza ziara yake mkoani Iringa.