Rais Samia awanyooshea kidole Ma DC

0
165

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wakuu wa wilaya nchini kuendelea kuchapa kazi, na kuachana na mawazo kuhusu mabadiliko yatakayofanyika.

Amesema amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya kupata taarifa kuwa kuna baadhi ya wakuu wa wilaya ambao hawafanyi kazi wakisubiri mabadiliko (Mkeka).

“Nimepata taarifa wengine hamfanyi kazi mnasubiri mkeka, kazi ya kutoa mkeka ni yangu mimi, nitatoa ninapotaka”, amesema Rais Samia

Amewaagiza wakuu wote wa mikoa kumpatia taarifa ya utendaji kazi wa wakuu wa wilaya ili atakayeonekana hafanyi kazi akisubiri mkeka aondolewe.

Rais Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kutia saini mkataba wa usimamizi wa shughuli za lishe.

Mkataba huo umetiwa saini baina ya Rais Samia Suluhu Hassan na Wakuu wa mikoa ya Tanzania Bara.