Rais Samia atoa pole vifo vya watu 17

0
135

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa wafiwa na wote walioguswa na vifo vya watu 17 waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Magila Gereza, tarafa ya Mombo wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Dkt. Samia amewaombea marehemu wote wapumzike mahali pema na majeruhi wapone haraka.

Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso na basi dogo aina aina ya Coaster.

Katika ajali hiyo watu wengine 12 wamejeruhiwa.