Rais Samia atoa bilioni 60 za Korosho

0
189

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewahakikishia wakulima wa zao la korosho kutokatwa fedha za pembejeo sababu tayari serikali imetoa bilioni 60 kwaajili ya pembejeo.

Amesema hayo akiwa mkoani Mtwara wakati ziara ya Sekretarieti ya CCM Taifa  katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Njombe.

Chongolo amefafanua kuwa, miaka ya nyuma serikali ilikuwa ikitoa bilioni 50 kila msimu  ambapo wakulima walikuwa wakikatwa fedha hizo pindi wanapoenda kuuza korosho zao.

Amesema, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 60 kwa ajili ya pembejeo mwanzo wa msimu ili kuwasaidia wakulima kupata faida kubwa na hakutokuwa na makato kama ilivyokuwa awali.

Aidha, Chongolo ameelez kuwa kwa mwaka huu Rais Samia ameelekeza Korosho zote kupakiwa katika bandari ya Mtwara na sio ya Dar es Salaam kwaajili ya kusafirishwa, kwani bandari hiyo imegharimu shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya upanuzi ili kuiongozea uwezo na kuwanufaisha wakulima wa mikoa ya kusini.