Rais Samia Suluhu Hassan ameteua Majaji wanne wa Mahakama ya Rufani na Majaji Ishirini wa Mahakama Kuu, uteuzi ulioanza Septemba 03, 2023.
Majaji wa Mahakama ya Rufani walioteuliwa ni
Jaji Lameck Mlacha ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kigoma na Jaji Paul Ngwembe ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Morogoro.
Wengine walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama.ya Rufani ni Mustafa Kambona Ismail ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu, Dar es Salaam na Jaji Abdul-Hakim Ameir Issa ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Zanzibar.
Majaji wa Mahakama Kuu walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni
Dkt. Evaristo Longopa ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Amemteua Wilbert Chuma kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Chuma alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Rufani Dar es Salaam.
Amemteua Sharmillah Said Sarwat kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Sarwat alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
Amemteua Arnold Kirekiano kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi Kirekiano alikuwa Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
Amemteua Martha Mpaze kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Mpaze alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Jumuishi katika Masuala ya Mirathi na Familia, Dar es Salaam.
Amemteua Ferdinand Kiwonde kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Kiwonde alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu.
Amemteua Said Ding’ohi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Ding’ohi alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Iringa.
Amemteua Dkt. Angelo Rumisha kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Rumisha alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
Amemteua Sarah Mwaipopo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.
Amemteua Ntuli Mwakahesya kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Mwakahesya alikuwa Naibu Karani wa Baraza la Mawaziri, Ofisi ya Rais Ikulu, Dodoma.
Amemteua Griffin Mwakapeje kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Mwakapeje alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Wizara ya Katiba na Sheria, Dodoma.
Amemteua Dkt. Dafina Ndumbaro kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Ndumbaro alikuwa Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dodoma.
Amemteua Emmanuel Kawishe kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Kawishe alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dodoma.
Amemteua Abdallah Halfan Gonzi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Gonzi alikuwa Mjumbe wa Baraza la Rufani za Kodi (TRAT) na Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Amemteua Kamazima Kafanabo Idd kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi Idd alikuwa Mhadhiri Msaidizi Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM), Dar es Salaam.
Amemteua Frank Mirindo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Mirindo alikuwa Mhadhiri Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Tanga.
Amemteua Hadija Kinyaka kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Kinyaka alikuwa Wakili wa Kujitegemea Kampuni ya Uwakili ya Lawhill Co. & Advocates, Dar es Salaam.
Amemteua Aisha Ally Sinda kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi Sinda alikuwa Wakili wa Kujitegemea Kampuni ya Uwakili BOWMANS Tanzania, Dar es Salaam.
Amemteua Hussein Salum Mtembwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Mtembwa alikuwa Wakili wa Kujitegemea na Mmiliki wa Kampuni ya Uwakili ya HM Noble Attorneys, Mtwara.
Amemteua Irene Musokwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya uteuzi huo Musokwa alikuwa Wakili wa Kujitegemea na Mshiriki katika Kampuni ya Uwakili ya FC Attorneys, Dar es Salaam.