Rais Samia: Ateua mabalozi, mkuu wa chuo na mtendaji Mkuu

0
159

Rais Samia Suluhu Hassan, hii leo Agosti 17, 2021 amefanya uteuzi wa viongozi watakaoenda kushika nyadhifa za mbalimbali serikalini.

Rais Samia amemteua Jaji Mstaafu, Mohamed Chande Othman kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU).

Pia, amemteua Prof Elisante Ole Gabriel kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Prof. Ole Gabriel alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (mifugo).

Prof. Ole Gabriel anachukua nafasi ya Mathias Kabunduguru ambaye amestaafu. Ole Gabriel ataapishwa Agosti 21, Ikulu jijini Dar es Salaam pamoja na mabalozi wateule watatu ambao ni;

Balozi mteule, Luteni Jenerali Yakub Hassan Mohamed kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, balozi mteule Mahmoud Thabit Kombo kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia na balozi mteule Elsie Sia Kanza kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.