Rais Samia ateta na Waziri Mkuu (Mst) wa Uingereza

0
220

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza, Tony Blair, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Tony Blair ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Mabadiliko Ulimwenguni (Tony Blair Institute for Global Change) amemshukuru na kumhakikishia Mhe. Rais Samia kuwa taasisi yake inaunga mkono jitahada mbalimbali anazochukua katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.

Amesema ili kuwa na mafanikio ya haraka katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni muhimu kuwa na taarifa sahihi ambazo zitawezesha ufuatiliaji wa karibu wa miradi hiyo.

Kwa upande wake Rais Samia amemshukuru Mhe. Tony Blair kwa kukutana nae na kumjulisha ufuatiliaji na uratibu wa masuala yanayofanywa na taasisi yake katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania.

Aidha, Rais Samia amesema kwa sasa Serikali inaendelea na utekelezaji wa vipaumbele vyake kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.